Shirika la Dyslexia linalenga kutoa mafunzo kwa walimu shuleni

Shirika la Dyslexia linalenga kutoa mafunzo kwa walimu shuleni

Huku kampeni ya kufahamu ugonjwa dyslexia ikifanyika mwezi huu, shirika la dyslexia chini kenya limeshirikiana na chuo kikuu cha mount kenya katika kutoa mafunzo kwa walimu, wazazi na jamii yote kwa jumla kupitia kozi ya dyslexia ili kuelewa jinsi ya kuwafunza wanafunzi wanaopitia ugumu katika kusoma na kuandika shuleni.Akizungumza wakati wa 2024 kongamano la africa dyslexia summit lilofanyika katika chuo kikuu cha mku, phyllis munyi ambaye ni mwanzilishi wa shirika hili ametaja baadhi ya mbinu wanazotumia katika shule ya rare gem talent iliyoko kitengela katika kuwaelimisha wanafunzi. Kwa upande wake, agustine mumo ambaye ni mwalimu katika shule hiyo, ameeleza changamoto wanazopitia katika kutekeleza juhudi za kuelimisha, huku akitoa wito kwa walimu kujielimisha zaidi kuhusu hali hii